Unaweza kusema ndani ya Simba eneo la beki wa kati mwenye namba yake yupo njiani kutua kikosini hapo baada ya klabu hiyo kufikia dau linalotakiwa na Coastal Union kwa ajili ya kumuachia Lameck Lawi (18).
Uongozi wa Coastal ulisisitiza kuwa bila ya Sh 200 milioni, beki huyo mwenye umri wa miaka 18 hataenda popote na badala yake atabaki klabuni hapo kumalizia mkataba wa miaka miwili uliosalia. Simba imekubali kulipa kile ambacho timu inayommiliki mchezaji huyo inakitaka ili ipate huduma yake msimu ujao.