Mchezaji Aziz K Ateuliwa Mchezaji Bora Mwezi wa Nne

Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Stephane Aziz Ki ameteuliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Aprili 2024, kwenye NBC Premier League huku kocha wa timu hiyo Miguel Gamond akiteuliwa kuwa Kocha Bora.

Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Aziz Ki ameibuka Mchezaji Bora akiwashinda Kipre Junior wa Azam FC na Joseph Guede wa Yanga.

Kwa upande wa Gamond, yeye amewashinda Bruno Ferry wa Azam FC na Malale Hamsini wa JKT Tanzania.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii