Trump aahidi akichaguliwa atarejesha marufuku ya kusafiri kwa baadhi ya nchi zenye waislamu wengi duniani

Mgombea anayaetarajiwa kuwa mteule wa urais wa kupitia chama cha Republican Donald Trump anasema akichaguliwa atarejesha tena marufuku ya kusafiri kwa baadhi ya nchi zenye waislamu wengi katika siku ya kwanza ya utawala wake mpya.

Marufuku ya kusafiri ilikuwa sehemu yenye utata katika muhula wake wa kwanza kama rais na ilibatilishwa na Rais Joe Biden alipoingia madarakani.

Donald Trump alipowania urais mwaka wa 2016, aliahidi kubadilisha uhamiaji wa Marekani ili kuwazuia magaidi kutoka nchi za Kiislamu.

Akiwa madarakani, Trump aliweka marufuku ya kusafiri kuingia Marekani kutoka nchi saba zenye Waislamu wengi duniani

Na kuzua maandamano na changamoto za kisheria, ikijumuisha kutoka taasisi ya American Civil Liberties Union.

Marufuku ya kusafiri ilijadiliwa hadi katika Mahakama ya Juu ya Marrekani, ambapo wengi wa kihafidhina waliidhinisha katika hatua iliyosherehekewa na Trump mtandaoni na huko White House.

Joe Biden alifanya kampeni dhidi ya marufuku ya kusafiri ya Trump mnamo mwaka 2020. Na kukomesha marufuku hiyo alipokuwa rais.

Sasa miaka minne baadaye, Trump aliwaambia wafuasi huko Wisconsin wiki hii kwamba matukio katika Mashariki ya Kati yanamsadikisha kwamba ni wakati wa marufuku mengine ya kusafiri.

Katika kampeni hii, Biden ametetea michango ya wahamiaji kwa Marekani, akiambia kundi la wafadhili wa kampeni wiki hii kwamba nchi zingine zimeteseka kwa sababu zinachukia wageni.

Kura ya maoni ya mwezi Aprili ya Harvard CAPS-Harris inaonyesha kuwa uhamiaji na mfumuko wa bei kama masuala makuu kwa wapiga kura wa Marekani.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii