DEBLINKZ ni wasanii wawili walioamua kuungana Pamoja na kutengeneza kundi la muziki kutoka nchini Nigeria Wakiwa wanafahamika kwa majina halisi kama Onyekachi na Onyebuchi Ikeh kutoka jimbo la Anambra, wawili hao wakubwa wa Kiafrika walianza safari yao ya kikazi mwaka wa 2006.
Wakianzisha lebo yao wenyewe, C-unit Management, ambayo zamani ilijulikana kama DEBLINKZ, wawili hao wamezua gumzo katika tasnia ya muziki mara kadhaa.