Chama Apewa Zawadi ya Kitimoto

Shabiki wa Simba Simon Mkondya ambaye ni Mfanyabiashara na Mfugaji kutoka Jijini Dodoma ( 104.4), amemtaka Wachezaji wa Simba Clatous Chama na Kibu Dennis kwenda kuchukua zawadi ya Nguruwe shambani kwake ikiwa ni ahadi yake ya kutoa Nguruwe mmoja kwa kila goli Simba watakalofunga.


“Kibu Dennis na Chama tumeona tuwapatie Nguruwe mmoja mkubwa ambaye ana mimba, mwenye kilo 500 ambaye atazaa Watoto 21 mwezi wa sita wao watajua wanagawana vipi.


"Nguruwe anazaa kwa mwaka mara tatu ni sawa na Nguruwe 63 ambao wakiweza kuishi kwa muda wa miezi sita kila Nguruwe anauzwa shilingi milioni moja kwa maana ni kwamba watakwenda kupata zaidi ya milioni 63,” amesema Mkondya.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii