Kenya imewarudisha raia wawili wa Uingereza nchini humo ambako wanasakwa kwa mauaji.
Taarifa kutoka kwa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya inasema wapelelezi walimkamata Mohamud Siyad Abdihakim, 24 na Monteiro Tariq Kennedy Mangal, 21, katika mtaa wa Kilimani jijini Nairobi wiki iliyopita kufuatia taarifa za kijasusi.
Polisi wanasema waranti ya kimataifa ya kuwakamata likuwa imetolewa dhidi yao kufuatia mauaji ya mwaka 2019 ya mvulana wa miaka 16- aliyetambuliwa kama Alex Smith, ambaye alichomwa kisu hadi kufa mjini Camden.
Polisi wanaamini mmoja wa watoro hao waliokamatwa ndiye iliyekeleza mauaji hayo, na mwingine alikuwa kwenye mojawapo wa magari mawili yaliyoibwa wakati wa tukio hilo, ambalo lilikuwa limeripotiwa kutokana na uhasama kati ya magenge mawili ya uhalifu.
Maafisa wa upelelezi wanasema Tariq alipatikana akiwa na kitambulisho cha Kisomali kilichokuwa na jina la Abdulahi Abshir Mohamed na njora.
Wanaume wengine tayari wanahudumia vifungo vyao nchini Uingereza kufuatia majukumu yao katika mauaji hayo.