Dani Alves Ahukumiwa Kifungo Cha Miaka Minne Na Miezi 6 Jela

NYOTA wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil, Dani Alves amehukumiwa kifungo cha miaka minne na miezi 6 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumnyanyasa kingono mwanamke mmoja katika klabu ya usiku ya Barcelona mnamo mwaka 2022.

Uamuzi huo umefanywa na Mahakama kuu Nchini Uhispania ambayo sambamba adhabu hiyo imemuamuru beki huyo wa zamani wa Barcelona alipe euro 150,000 kwa mwathirika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii