Meek Mill amewauliza swali lingine mashabiki wake kuhusu Afrika, lakini safari hii ni kuhusu wasanii gani kutoka bara hilo anatakiwa kufanya nao kolabo. Akitumia Twitter/X Jumanne (Januari 30), Meek aliomba jina ambalo angetengeneza albamu nzima - na akaahidi kuwa ataimaliza ndani ya wiki mbili pekee.
"Kama ningetengeneza albamu na msanii wa Kiafrika iwe nani???" Aliuliza. "Swali kwa Nigeria Ghana? Ninarap vizuri ningeweza kufanya ndani ya wiki 2 na mtayarishaji mzuri ??? Acha maoni ya nani??
Ikumbukwe meek mill aliwahi kufanya kolabo na davido mwaka 2015 kupitia wimbo wa fans me ambao unapatikana katika album ya davido baddest .