Real Madrid imetajwa kuwa klabu ya soka iliyoingiza mapato ya juu zaidi duniani kwa msimu wa 2022/23 kwa mujibu wa Deloitte Sports Business Group, ikichukua nafasi ya Manchester City iliyokuwa kileleni mwa orodha hiyo.
Deloitte Football Money iko katika mwaka wake wa 27 wa kuchanganua klabu za kandanda zinazoingiza mapato ya juu zaidi duniani, na iliripoti Madrid ilipata rekodi ya euro bilioni 10.5 katika msimu wa 2022-23, sawa na ongezeko la asilimia 14 kutoka mwaka jana.
Madrid kwa mara ya mwisho walikuwa kileleni mwa orodha hiyo miaka mitano iliyopita, na waliripoti rekodi ya euro milioni 831 kwa kipindi cha msimu uliopita, zaidi ya mwaka uliopita.
City walipata pungufu ya euro milioni tano kuliko Madrid katika nafasi ya pili, huku tano bora wakijazwa na Paris Saint-Germain (euro milioni 802), Barcelona (euro milioni 800O) na Manchester United (euro milioni 746).
Kupanda kwa PSG na Barca katika tano bora kunaonyesha klabu za Ulaya “kurejea” kwenye himaya dhidi ya zile za Ligi Kuu England, kwa mujibu wa Deloitte, ingawa Liverpool, Arsenal, Chelsea na Tottenham Hotspur zote zipo kwenye 10 bora.
Liverpool ndio walioshuka daraja katika orodha hiyo, wakitoka nafasi ya tatu hadi ya saba, kutokana na kushuka kwa matokeo katika michuano ya ndani na Ulaya.