Prof. Ndalichako: Maboresho Sheria Ya Fidia Kwa Wafanyakazi Yaja

SERIKALI imewahakikishia Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, kuwa inayachukulia kwa uzito mkubwa, maoni na mapendekezo yao kuhusu maboresho ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, wakati akifunga Kikao Kazi cha Mafunzo ya Uelimishaji kwa Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Kanda ya Kusini na Watendaji wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) mjini Songea, Februari 10, 2024.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii