Toko Ekambi astaafu Cameroon

Mshambuliaji Karl Toko Ekambi ametangaza rasmi kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Cameroon baada ya kuondoshwa katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Afcon 2023 na Nigeria kwa kichapo cha magoli 2-0 nchini Ivory Coast. 


Toko Ekambi mwenye umri wa miaka 32 anayeitumikia klabu ya Al-Ettifaq ya nchini Saudi Arabia ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema nimehuzunishwa na kutofika mbali lakini najivunia kwa uwezo wa timu yangu kwa pamoja,ukurasa wa shindano la 4 la Afcon umefungwa na mwisho wa historia yangu ndani ya Cameroon.

Karl Toko Ekambi ameitumikia timu yake ya taifa kwa kipindi cha miaka 9 kuanzia mwaka 2015 mpaka 2024 huku ameitumikia Cameroon kwenye michezo 60 na kufunga magoli 15 sambamba na kutwaa ubingwa wa Afcon 2017 nchini Gabon.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii