DRC yafanya Uchaguzi Mkuu

Takriban wapiga kura milioni 44 wameitwa kumchagua rais wao lakini pia wabunge wao wa kitaifa na mikoa na madiwani wao wa manispaa leo Jumatano. Rais anayemaliza muda wake, FĂ©lix Tshisekedi, anatafuta muhula wa pili wa miaka mitano akikabiliana na upinzani uliogawanyika.


Wapiga kura wanaendelea kumiminika katika vituo vya kupigia kura mjini Kinshasa na katika baadhi ya maeneo mengine nchini, huku uchaguzi mkuu nchini DRC ukiendelea.

Hata hivyo zoezi lenyewe limechelewa kuanza katika vituo vingi huku maafisa wa tume wakiendelea na harakati za kufanya maandalizi

Idadi ndogo ya wapiga kura ilijitokeza katoka vituo vingi lakini idadi hii inatarajiwa kuongezeka kadri siku inavyosonga mbele.

Rais Felix Tshisekedi ambaye anawania muhula wa pili anatarajiwa kupiga kura yake wakati wowote kuanza sasa mjini Kinshasa.

Naye mgombea wa upinzani Martin Fayuku anatarajiwa kupiga kura yake mwendo wa saa tatu asubuhi huku mgombea Moise Katumbi akitarajiwa naye kupiga kura yake mwendo wa saa tano asubuhi.

Wakati huo huo mamlaka ya usafiri wa anga imetangaza kufunga mipaka ya nchi kavu na baharini kwa saa 24 kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu unaofanyika leo Jumatano.

Kulingana na Kurugenzi Kuu ya Uhamiaji, mipaka itafungwa kuanzia Jumatano asubuhi hadi saa 11:59 jioni kwa saa za ndani siku hiyo hiyo.

Anga ya Congo pia itafungwa kwa safari za ndani ambazo hazijaidhinishwa, lakini safari za ndege za kimataifa zitaendelea kama kawaida, kurugenzi ilisema katika taarifa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii