Watu nane wamefariki Dunia na wengine thelathini na moja kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani wa Kilimanjaro, Mrakibu Msaidizi Jeremiah Mkomagi alisema kuwa, tukio hilo limetokea leo majira ya asubuhi katika barabara ya Ugweno.
Amesema, Basi kampuni ya Mvungi lililokuwa likitokea Vuchama Ugweno kuelekea jijini Dar es salaam lilipokuwa likilikwepa gari dogo ndipo lilienda pembezoni mwa ngema ya mlima ambapo uzito uliizidi ngema na kupelekea kuanguka bondeni.
“Kama unavojua kipindi hiki ni cha mvua sasa dereva wa hili basi alikuwa analikwepa gari dogo akawa ameenda pembeni ya kingo ya mlima ndipo uzito ulipolea na kupelea kuangukia bondeni,” alisema Mkomagi.
Ameongeza kuwa, watu saba walifariki Dunia papo hapo huku mmoja akifariki wakati anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Kanda ya KCMC na wengine 31 kujeruhiwa na walikimbizwa katika hospitali ya Kifula na KCMC, Kilimanjaro.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Kanda ya KCMC, Gabriell Chiseo amethibitisha Hospitali hiyo kupokea majeruhi saba akisema wa kike ni wanne na wakiume watatu.
Chiseo alisema kuwa, kati ya majeruhi hao mmoja ambaye ni Mwanamke alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu na majina ya waliofariki i kama inavyojionesha katikia kiambata.