EFA yawaangushia lawama wachezaji

Shirikisho la Soka Misri ‘EFA’ limewatupia lawama wachezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo ‘The Pharaoh’ baada ya timu hiyo kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Msumbiji katika mchezo wa Kombe la Mataifa ya ‘AFCON 2023’ juzi Jumapili (Januari 14).

Misri ambao ni mabingwa wa kihistoria wa taji hilo, ndio walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Mostafa Mohanmed dakika mbili tangu kuanza kwa mhezo huo.

Hata hivyo, Penati ya dakika za mwisho iliyowekwa kimiani na nyota wa Liverpool, Mohamed Salah ilitosha kuiokoa Misri na kipigo na kuifanya timu hiyo kuanza kwa sare katika fainali hizo zinaoendelea nchini Ivory Coast.

Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Misri ‘EFA’, Khaled El-Da-randaly, alibainisha kuwa wachezaji wao hawakuwajibika inavyotakiwa katika mchezo huo na ndio maana walishindwa kuibuka na ushindi.

Kiviwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Soka ‘FIFA’ vya mwezi  Desemba 2023, Misri iko katika nafasi ya 33 wakati Msumbiji wanashika nafasi ya 111.

Misri pia ndio timu inayoongoza kwa kutwaa mara nyingi taji la ‘AFCON’ baada ya kulibeba mara saba wakati Msumbiji haijawahi kulibeba.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii