Miss Ardhi University Yafanya Kufuru, Mshindi Azawadiwa Kiwanja

Dar es Salaam 14 Januari 2024: Shindano la kumsaka Miss University mwaka huu lililofanyika Ukumbi wa Mirado uliopo Sinza Dar usiku wa kuamkia jana (Jumapili) limetajwa kuyafunika mashindano mengine yote yaliyowahi kufanyika chuoni hapo siku zilizopita kwa ubora na kujaza umati mkubwa wa wahudhuriaji.

Katika kinyang’anyiro hicho msomi, Debora Lovebond ndiye aliyeibuka na taji la Miss Ardhi University huku wenzake 11 wakiondoka na mataji mbalimbali ya vipaji na ubunifu.

Kwa kutwaa taji hilo, Debora amepewa zawadi ya kiwanja kutoka Kampuni ya Eldad Property Limited waliokuwa wadhamini wa shindano hilo.

Akizungumza baada ya kinyang’anyiro hicho, Rais wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Innocent Alex alimpongeza Debora na washiriki wenzake wote kwa kushiriki kinyang’anyiro hicho pamoja na waliojishindia tuzo za talent mbalimbali.

Alex amesema Debora ametwaa taji hilo lakini waliomfuatia pia nao wamefanya vizuri ndiyo maana wakafikia hatua ya fainali hizo hivyo nao wajivunie ushiriki huo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii