Mwanadada selena Gomez ambaye ni mwimbaji kutoka nchini marekani amekuwa akiandika vichwa vingi vya Habari katika matukio mbali mbali lakini karibuni alifunga midomo ya watu wengi baada ya kutangaza kuwa ameanguka katika penzi zito na msanii mwenzake aitwae benny blanco ambao ni watu wanaoonekana wamezama katika mahaba mazito.
Wikiendi iliyopita selena alihudhuria katika usiku wa tuzo za golden globe ambazo zilihudhuriwa na watu mbali mbali maarufu lakini inawezekana siku hiyo haikuwa nzuri kwa selena Gomez baada ya video kadhaa kuonyesha mwigizaji timothee akizungumza jambo ambalo sura yake ilionyesha kukataa kutokana na selena alichomwambia na baadae selena alionekana akiwa anazungumza na Rafiki yake wa karibu ambaye taylor swift huku katika video hiyo taylor swift alionekana kushangazwa na maelezo ya selena Gomez.