DUA LIPA SIPENDI MTU ANAYEKULA MDOMO WAZI.

Mwanadada ambaye alitamba na wimbo wa new rules dua lipa ambaye amefanikiwa kufanya vizuri na kufikia chati mbali mbali za muziki duniani kwa kazi zake ikiwemo levitate 

Kwa mara nyingine dua lipa ameibuka na kuweka wazi moja ya vitu ambavyo hapendezwi navyo kwenye hekaheka za kila siku na kudai kuwa hapendi kabisa mtu ambaye anatafuna chakula huku ameacha mdomo wake wazi ni moja ya jambo ambalo linamkera sana mara nyingi.

Ameyasema hayo akiwa katika mahojiano na chombo kimoja cha Habari nchini marekani na kudai kuwa moja ya kitu asichopenda ni kuona mtu anatafuna chakula mdomo wazi Pamoja na mtu anayevaa soksi fupi fupi sana mgunii.

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii