Zarinah hassan maarufu kwa jina la zari the bosslady ambaye amekuwa akiingia katika vichwa vya Habari mbali mbali ,zari inafahamika hapa nchini Tanzania amewahi kuwa na mahusiano na mwanamuziki diamond platnumz na wakabarikiwa kupata Watoto wawili Pamoja ambo ni tiffah Pamoja na nilan.
Kwa hivi sasa zari yuko katika ndoa na kijana kutoka nchini kwao Uganda ambaye anafahamika kwa jina la shaqib.
Hivi karibuni zari alifanya show ya white party nchini Rwanda ambapo alifanikiwa pia kufika katika vyombo mbali mbali vya Habari na kufanya mahojiano lakini moja ya swali ambalo aliulizwa ni kama mtu maarufu amewahi kupitia hali ya msongo wa mawazo na zari alijibu:,
“ni kweli kabisa na ni kitu halisia kipo na kinatesa sana mume wangu alipofariki wiki tano baadae mama yangu nae akafariki ni moja ya jambo ambalo lilinisumbua sana na nikawa sioni hata mtu wa kumelezea shida yangu kwahiyo nilikuwa nalia sana mpaka ikafikia hatua ya mimi kubadili chumba change cha nguo kuwa chumba maalumu cha kufanyia sala kwa mwezi mzima nilikuwa naamka saa tisa usiku kusali na kumlilia mungu aniweke sawa kulingana na namna nilivyokuwa najisikia na kweli nilifanikiwa kwahiyo hata wewe unayepitia hali hiyo unaweza pia”
Alisema zari ambaye alisisitiza kuwa watu wengi wanaomuona mtandaoni hudhani wameyajua Maisha yake asilimia zote lakini kiuhaliasia ni kipande kidogo sana ambacho ameamua kuonyesha watu.