Jay Z "Ni Ubinafsi niki-performe Super Bowl"

Producer na mshirika wa biashara wa Super Bowl halftime shows Shawn Carter Jay Z ‘HOV’ amesema anahisi atakuwa mbinafsi kama akijichagua mwenyewe kuperforme show hiyo ya Super Bowl.

"Kuwa stejini kuperforme Super Bowl sijajua, nahisi itakuwa ubinafsi kujichagua mwenyewe. Ni mapema sana labda mwaka mmoja” amesema #JayZ kupitia Entertainment Tonight.

Super Bowl Halftime show ya mwaka huu 2024 itatumbuizwa na Usher Raymond. Pia rapa Lil Wayne ametangaza kutamani kuperforme show hiyo mwaka 2025.
 


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii