Bondia Hassan Mwakinyo ( @hassanmwakinyojr ) amesema Shirikisho la Mchezo wa Ngumi Duniani (WBO) limeridhia kwamba pambano lake la January 27,2024 New Amaan Complex Zanzibar litakuwa la kuwania ubingwa wa WBO Africa na kwamba sasa atapigana na Bondia Miya NKanku kutoka Congo Katika round 10 uzito wa kilo 72 badala ya Mzimbabwe Enock Msambuzi.
“Message kwako Erick Msambudzi nasikitika
27/01/2024 New Aman Complex Indoor Zanzibar sitaweza kucheza nawe kwasababu ya taratibu za Wasimamizi wa ngumi Duniani ingawa nilikupania na ulikuwa daraja moja jepesi kulivuka lakini nina furaha kuwajulisha Watanzania wenye mapenzi mema na maendeleo ya mchezo ile fursa na ndoto ya kupigania mkanda mkubwa Duniani imepatikana”