Msanii wa muziki kutoka nchini nigieria ambaye kwa nafasi yake amefanikiwa kufanya vizuri katika majukwaa mbali mbali ya muziki ambayo kwa namna moja ama nyingine yamefanya jina lake kukua kwa kiwango kikubwa ndani ya muda mfupi akiwa na kazi kali kama vile bloody Samaritan,rush,na nyingine nyingi.
Ayra starr ni msanii ambaye umri wake Pamoja na umaarufu vimemfata kaiwa bado mchanga sana kimaaamuzi na kadhalika jambo ambalo wengi huwasumbua katika kujisimamia lakini kwa ayra starr anasema hajawahi kutetereshwa na suala la kuwa maarufu kwani umaarufu umefata akiwa yeye kama yeye bila kumuiga mtu yeyote ayra starr ameyasema hayo akizungumza na chanzo kimoja cha Habari huko nchini marekani na kusema
“mimi nimefatwa na umaarufu kwa sababu nimekuwa mimi na siwezi badilika kwa namna yoyote ile kwakuwa hakuna kinachonifanya niige mtu mwingine kulingana na vile ambayo mimi ninafanya n ahata kama ikitokea najikumbusha mimi ni nani”alisema ayra starr ambaye anafurahi kuona anaweza kuihudumia vizuri sana familia yake katika kila hatua katika ubora wa hali ya juu.