Mwanamuziki wa Hiphop nchini Fareed Kubanda ‘Fid Q’ amefiwa na baba yake mzazi, Mzee Kubanda.
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, @therelfidq ameandika “Ninasikitika kuwataarifu ya kwamba.. mzee wangu, baba yangu, Mzee Kubanda ametangulia mbele ya haki,”
Fid Q ameeleza kuwa mazishi ya babaye yatafanyika kesho kijijini kwake Nasa mkoani Mwanza.