Mwimbaji Cassie amshutumu Puff Daddy kwa ubakaji na unyanyasaji

Msanii wa muziki wa rap Sean "Diddy" Combs ametuhumiwa kwa ubakaji na biashara ya ngono na mwimbaji wa kike.


Katika kesi iliyoonekana  mpenzi wa zamani Casandra Ventura alisema alikuwa amenaswa kwa muongo mmoja katika mzunguko wa unyanyasaji na vurugu.


Bw Combs - ambaye pia amejulikana kwa jina la kisanii Puff Daddy - anakanusha madai hayo, akimshutumu mwimbaji huyo kwa kujaribu kumlaghai.


Wakili wake alisema madai hayo ni "ya kuudhi na ya kuchukiza".


Bi Ventura - mwimbaji wa muziki wa R&B anayejulikana kwa jina la kisanii Cassie - anadai kuwa nyota huyo wa rap alimbaka na kumpiga kwa zaidi ya miaka 10 kuanzia alipokuwa na umri wa miaka 19.


"Baada ya kuwa kimya kwa miaka mingi, hatimaye niko tayari kusimulia hadithi yangu," alisema katika taarifa siku ya Alhamis

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii