Diamond Platnumz Kutambulisha Msanii Mpya wa WCB

Staa wa Bongo Fleva na CEO wa Lebo ya WCB Wasafi, Diamond Platnumz ametangaza rasmi kuwa alhamis November 16, 2023 atamtambulisha Mkali mwingine mpya ambaye amemwaga wino kwenye lebo hiyo.

Diamond amesema anatamani Watu waone kiasi gani Nchi hii imejaliwa vipaji ambapo amepost video inayomuonesha akiwa na Wasanii wengine wa WCB, viongozi wa lebo na Watu wengine kwenye timu yake ambapo kwa pamoja wamemmwagia sifa Msanii huyo mpya kwa jinsi alivyo mkali wa kuandika, kuimba na muonekano bomba wa kisanii.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii