Mshambulizi wa Ghana Afariki Wakati wa Mechi huko Albania

Mchezaji soka wa Ghana Raphael Dwamena amefariki dunia kwa masikitiko baada ya kuzimia wakati wa mchezo wa Albania Superliga kati ya FK Egnatia na KF Partizani. 


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alianguka katika dakika ya 23 ya mchezo na kulazimika kukimbizwa hospitalini, ambapo ilitangazwa kuwa amefariki.

Dwamena amekuwa akicheza na Implantable Cardioverter-Defibrillator kutokana na tatizo la moyo. "Pumzika kwa Amani kwa mchezaji wa KF Egnatia Raphael Dwamena.

Ghanian alianguka uwanjani wakati wa mechi ya Superliga kati ya Egnatia na Partizani. Baadaye aliaga dunia hospitalini akiwa na umri wa miaka 28," iliandika Albania Footy, kuthibitisha kifo cha mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana. .

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii