Italia ya beba ubingwa baada ya miaka 47

Timu ya taifa ya Italia imeshinda ubingwa wa michuano ya tenisi ya Davis Cup baada ya kuifunga timu ya taifa ya Australia kwenye mchezo wa fainali uliochezwa Malga nchini Hispania jana usiku, ukiwa ni ubingwa wao wa pili wa michuano hii.

Wachezaji Jannik Sinner na Matteo Arnaldi ndio walioipa kombe hilo Italia baada ya kushinda michezo ya fainali. Matteo Arnaldi ndio alijuwa wa kwanza kucheza na akashinda kwa seti 2-1  dhidi ya Alexei Popyrin wa Australia kwa seti 7-5, 2-6 na 6-4  na kuitanguliza Italia kuongoza 1-0  kabla ya Sinner kushinda dhidi ya Alex de Minaur kwa seti 2-0 yani 6-3 na 6-0. 

Huu ni ubingwa wa pili wa Italia kwenye michuano hii n awa kwanza tangu mwaka 1976 hivyo huu ni  ni ubingwa wao wa kwanza wa Davis baada ya miaka 47 kupita ngau walipochukua mara ya mwisho.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii