Watumishi wawili wafukuzwa kazi, ulevi watajwa

Baraza la madiwani la manispaa ya Songea limewafukuza kazi watumishi wawili wa manispaa hiyo mmoja akiwa na tuhuma za vitendo vya ulevi ambavyo vimesababisha kuwa mtoro kazini na mwingine amefukuzwa kazi kwa kosa la kuwa na vyeti feki.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kumaliza kikao cha baraza la madiwani Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Michael Mbano amesema baraza lilikaa kama kamati na kuwajadili watumishi wawili wa manispaa hiyo na maazimio ya baraza hilo ni kuwafukuza watumishi hao ambapo mtumishi mmoja amefukuzwa kwa kosa la kuwa mlevi na kusababisha utoro kazini na mwingine amefukuzwa kwa kosa la kuwa na vyeti feki.

Watumishi hao ni Karence Ndunguru ambaye alikuwa msaidizi wa afya mwandamizi ambaye anatuhumiwa kwa vitendo vya ulevi na kwa muda mrefu hayupo kazini 

Mtumishi mwingine ni Josepha Mahonge ambaye anakesi ya kuwa na cheti feki na baada ya kuthibitika baraza limemfuta kazi.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii