Serikali ya Uingereza imesema itakutana na maafisa nchini Uturuki kujadili kanuni kuhusu utalii wa kimatibabu na urembo, baada ya vifo kadhaa kutokea.
Melissa Kerr, 31, alifariki dunia katika Hospitali binafsi ya Medicana Haznedar mjini Istanbul 2019 wakati wa upasuaji wa kuongeza makalio BBL
Uchunguzi wa maiti Uliibua wasiwasi kuwa ni kwasababu yeye na wengine hawakupewa taarifa za kutosha kabla ya kusafiri nje ya nchi na kuhusu upasuaji huo.
Agosti 2020 mama mmoja wa watoto watatu alifarki baada ya kufanyiwa upasuaji wa wa kurekebisha mwili nchini Uturuki na hapo awali BBC iliripoti jinsi wagonjwa saba wa Uingereza walivyofariki baada ya upasuaji wa kupunguza uzito katika nchi hiyo.
Uingereza imekubali kusitishwa kwa upasuaji wa aina hiyo kutokana na hatari zinazohusika.
"Maafisa wa Idara ya Afya watatembelea Uturuki hivi karibuni kukutana na wenzao". alisema Waziri wa afya.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii