Mtoto wa Rais achaguliwa kuwa mgombea mwenza

Waziri wa ulinzi wa Indonesia na mgombea wa urais, Prabowo Subianto amemtangaza mtoto wa kiume wa rais anayeondoka madarakani, Joko Widodo kuwa mgombea wake mwenza katika uchaguzi unaotarajia kufanyika 2024.

Uchaguzi wa Gibran Rakabuming Raka (36), kuwa mgombea mwenza, unadaiwa kuwa unaweza kumpa nguvu Prabowo katika kampeni yake kutokana na umaarufu wa Widodo, licha ya  hasira za umma juu ya uamuzi wa Mahakama kubadilisha vigezo vya awali vya wagombea.

Indonesian President Joko Widodo gestures during an interview with Reuters at the Presidential Palace in Jakarta, Indonesia, February 10, 2016. Indonesia on Thursday opened dozens of sectors to foreign investors in what President Joko Widodo has described as a “Big Bang” liberalisation of its economy, Southeast Asia’s largest. Picture taken February 10, 2016. REUTERS/Darren Whiteside – RTX26FW2

Vigezo hivyo, vinasemekana huenda vingemzuia Gibran kugombea katika uchaguzi huo ambapo hata hivyo Indonesia itafanya uchaguzi mkuu wa Rais na Bunge Februari 14, 2024 huku waatu milioni 205 nchini humo kati ya raia wote milioni 270 wakiwa wamejiandikisha kushiriki uchaguzi huo. 

Hata hivyo, Rais Joko Widodo alikana kutohusika na wagombea wa urais, licha ya wajuzi wa mambo ya kisiasa kudai kuwa anataka kuendeleza ushawishi wake katika siasa za taifa hilo na inahisiwa amekuwa akimuunga mkono kwa siri mpinzani wake wa zamani, Prabowo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii