Wito huo umetolewa  Afisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Charles Maguzu, wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Taifa ya kuogelea kwa watu wenye Ulemavu yaliyofanyika kwenye Bwawa la Gymkhana Dar es Salaam.

Aliongeza kwa kuwataka wazazi wenye watoto wa kundi hilo wasiwafiche au kuwazui kushiriki michezo bali wawatoe waweze kushiriki na kuonyesha vipaji vyao.

"Watu wenye Ulemavu ni watu kama sisi tusio na Ulemavu na wana haki ya kushiriki shughuli za kujenga uchumi wa taifa letu," amesema  Maguzu.

Maguzu amesema  kuwa washiriki hao wasikate tamaa na waendelee kuwasikiliza makocha wao na ikiwezekana ndani ya mwaka huu au mwakani kuwe na timu ya kuogelea ya watu wenye ulemavu ili iwakilishe nchi katika mashindano ya Afrika na nje ya Bara la Afrika.

"Nawapongeza wadhamini waliojitokeza na wengine ambao wana nia waje kusaidia kuandaa na kama yupo mdhamini anayetaka aende BMT waweze kushirikiana kumfikia," amesema .

Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha waogeleaji wa kundi hilo, Thauriya Diria, amesema  kuwa bado wanahitaji udhamini Ili waweze kuwakuza wachezaji kuwaendeleza wachezaji hao Ili waweze kushiriki mashindano na mwaweze kupata leseni Ili kujua madaraja ya wachezaji yao.

'' Wataendelea kuwafundisha na kuwakuza wachezaji Ili kupata wawakilishi wa nchi kimataifa ''Diria

Kwa upande wa Katibu Mkuu Chama Cha Kuogelea Zanzibar(TSA) Said Nassor aliwapongeza TPSA kwa kutambua umuhimu wa Tanzania kuwa inajenga pande mbili Bara na Zanzibar na kushirikiana katika mashindano hayo.