Andrè Onana kusugua benchi Man Utd

Imeripokuwa kuwa Kocha Mkuu wa Manchester United, Erik ten Hag, anafikiria kumuweka nje kipa namba moja wa timu hiyo, Andrè Onana.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuonekana Onana kukosolewa mara kwa mara kutokana na kuruhusu mabao mengi tangu ajiunge na timu hiyo msimu huu.

Onana ambaye ametua Man United kwa uhamisho wa Pauni 54m akitokea Inter Milan, alitarajiwa kuwa mrithi sahihi wa David de Gea, lakini mpaka sasa ameonekana kuwa na makosa mengi golini.

Kipa huyo katika mechi 11 za michuano yote alizodaka msimu huu, ameruhusu mabao 19, huku akiwa na clean sheet tatu.

Wakati Ten Hag akifikiria kumpiga benchi Onana, kipa namba mbili wa kikosini hicho ambaye naye amesajiliwa msimu huu, Altay Bayındır, anatazamiwa kupewa nafasi kwani mpaka sasa hajacheza mechi yoyote.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii