Ed Sheeran ajichimbia kaburi lake la kuzikwa

Muimbaji na mwandishi wa nyimbo Uingereza na duniani Ed Sheeran tayari ameshajichimbia kaburi lake ambalo ikitokea siku amefariki atazikwa hapo.

Mshindi huyo wa tuzo 4 za Grammy amefichua hilo kupitia Interview aliyofanya na GQ Hype akisema "Nisingesema ni siri, ni shimo ambalo limechimbwa ardhini na jiwe juu yake, kwa hiyo siku yoyote inapofika na mimi kufa, ninaingia humo”.

Baadhi ya mashabiki mitandaoni wamempongeza Ed Sheeran kwa kujipanga na kujiandalia maisha mengine nje ya dunia.

Kibongobongo pia baba mzazi wa Cappuccino Tunda Mzee Kimaro tayari amejiandalia kaburi lake la kuzikwa Moshi, Kilimanjaro.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii