Kuna vita ya maneno inaendela chini kwa chini kati ya Drizzy Drake na rapa wa zamani Joe Budden ambaye ni mtangazaji kwa sasa nchini Marekani.
Vita hiyo imeanza baada ya Joe Budden kuikosoa Album mpya ya Drake 'For All the Dogs' akisema Drake ana-rap kwa ajili ya watoto anahitaji kuandika muziki kwa ajili ya watu wazima.
Drake amemjibu Joe Budden akimwambia yeye tayari amefeli kwenye muziki ambao ulikuwa unamlipia bili zake ndio maana amebadilisha carrier na kujifanya GOAT.
"Umestaafu kwenye muziki bila kuona jezi yako wala namba yako hatukumbuki, umekimbia kwenye rap sio kwa sababu umekamilisha yote unayohitaji bali umefeli". ameeleza Drake
Pia kwenye post yake mpya ya Drake amempiga tena dongo Joe Budden kuhusu kazi yake ya utangazaji baada kustaafu kurap akiandika "Ahsante Mungu kwa maisha sio kukimbilia haraka kununua mic bora zaidi kwa ajili ya Podcast".