Walinda usalama wamezingira afisi za upinzani

Maofisa wa polisi nchini Uganda na wenzao wa jeshi, wameripotiwa kuweka vizuizi katika afisi kuu za chama cha upinzani cha National Unity Platform (NUP), kinachoongozwa na mwanasiasa wa upinzani Bobi Wine.


Katika taarifa yake kwenye mtandao wa X, chama hicho kimethibitisha kuzuiliwa kwa afisi zake katiak eneo la Kamwokya.

Kwa mujibu wa kiongozi wa chama hicho, Bobi Wine, maofisa wa serikali wamevamia makao makuu ya chama chake na kwamba wamewazuia watu kuingia au kutoka kwenye majengo ya chama hicho.

Mwanamuziki huyo wa zamani ambaye kwa sasa ni  mwanasiasa aliandika kwenye  mitandao wake wa  kwamba hatua hiyo ya maofisa wa usalama inalenga kuzuia hafla ya maombi ambayo NUP ilikuwa imepanga kufanya katika ofisi yake Kampala siku ya Jumatatu.

Wiki iliyopita, polisi walimsindikiza Bobi Wine hadi nyumbani kwake baada ya kurejea Uganda kutoka Afrika Kusini, wakisema kuwa hatua hiyo ilikuwa ni kumzuia kuandaa maandamano.

Pia waliwazuilia makumi ya wafuasi wa Bobi Wine kwa madai kwamba walichochea vurugu na kupanga maandamano ambayo hayakuwa na kibali.

Bobi Wine amewakosoa maafisa hao wa usalama kwa hatua hiyo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii