Mkutabo wa mwaka wa IMF na Benki ya Dunia wafanyika Afrika

Wajumbe wa Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, na Benki ya Dunia kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 50 wanafanya mkutano wao wa kila mwaka katika ardhi ya Afrika huko nchini nchini Morocco.

Mkutano huo unaofanyika leo Jumatatu unakabiliwa na shinikizo la kufanya mageuzi kwa ajili ya kuyasaidia mataifa maskini yaliyoathiriwa na madeni na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kwa kawaida, IMF na Benki ya Dunia huwakutanisha mawaziri wa fedha kwenye mkutano wa kila mwaka na magavana wa benki kuu kila baada ya miaka mitatu nje ya makao makuu yaliyoko mjini Washington, Marekani.

Jiji la kusini mwa Morocco la Marrakesh lilipaswa kuwa mwenyeji wa mkutano huo mnamo mwaka 2021, lakini uliahirishwa mara mbili kwa s+ababu ya janga la UVIKO-19.

IMF na Benki ya Duniazilifanya mikutano barani Afrika mara ya mwisho mnamo mwaka wa 1973, ambapo Kenya iliandaa hafla hiyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii