Viongozi washinikizwa kujiuzulu Simba SC

Baadhi ya Mashabiki na Wanachama wa Simba SC wameanzisha kampeni katika mitandao ya kijamii wakishinikiza baadhi ya viongozi wa klabu hiyo waondoke (kujiuzulu) kwa kile wanachodai kuwa wao ndio chanzo cha Simba SC kufanya vibaya.

Kupitia mtandao wa kijamii wa X zamani Twitter mashabiki hao wametumia hashtag ya #MangunguTryagainOut kuchapisha (post) katika kurasa zao wakitaka Mwenyekiti wa Simba Murtza Mangungu na Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ wajiuzulu nafasi zao.

Kampeni hiyo imekuja muda mchache tu baada ya Uongozi wa Simba kutangaza kufikia makubaliano ya pande mbili ya kuvunja mkataba na kocha Roberto Oliveira (Robetinho) baada ya kufungwa magoli 5-1 na watani zao Young Africans.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii