Arsenal yajuta kumsajili Kai Havertz

Imefahamika kuwa Uongozi wa Klabu ya Arsenal unajutia uamuzi wa kumsajili Mshambuliaji kutoka nchini Ujerumani, Kai Havertz kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Ukiweka kando bao la ushindi alilofunga kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya mwaka 2021, Mshambuliaji huyo hakuwa na wakati mguu kwa miaka mitatu yote aliyokuwa kwenye kikosi cha Chelsea.

Kai alifunga mabao 32 na kuasisti mara 15 katika mechi 139 za michuano yote alizotumikia Chelsea na hapo Kocha Arsenal Mikel Arteta aliona zinatosha na kumnasa mkali huyo mwishoni mwa msimu wa 2022-23.

Arteta amembadili Havertz na kumtumia kwenye nafasi ya Kiungo Mshambuliaji ambayo ameshindwa kuitendea haki ipasavyo.

Arsenal ililipa Pauni 65 milioni kunasa saini yake, ilipomng’oa Stamford Bridge akiwa bado na mkataba wa miaka miwili.

Na tangu alipotua Emirates, Havertz mwenye umri wa miaka 24, amefunga bao moja na kuasisti moja tu kwenye Ligi Kuu England akiwa na Arsenal, huku akianzishwa mara 12 na tano akitokea benchi kwenye michuano yote.

Taarifa zinaelezakuwa, baadhi ya mabosi kwenye kikosi cha Arsenal hafurahishwi na kiwango cha Havertz na tayari wanaona walifanya kosa kubwa kumsajili ikiwa ni miezi mitatu tu imepita tangu aanze kuitumia timu yao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii