Tory Lanez Aendelea Kusota Gerezani, Rufaa Yake Yagonga Mwamba

Baada ya ‘timu’ ya wanasheria wa ‘rapa’ Tory Lanez kutoka Canada kupeleka ombi la kumuachia msanii huyo kwa dhamana huku wakisubiri rufaa, ombi hilo limekataliwa.


Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Mahakama ya rufaa California, Meghan Cuniff, amedai kuwa mahakama hiyo haijamruhusu na imekataa Tory Lanez kutoka gerezani kwa dhamana.


Tory Lanez mwenye umri wa miaka 31 anatumikia kifungo cha miaka 10 baada ya kumpiga risasi aliyekuwa mpenzi wake Megan Thee Stallion, mguuni mwaka 2020 pamoja na makosa mengine mawili.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii