Mama Mbappe amuanika hadharani Mwanaye

Mama wa Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa PSG Kylian Mbappe amefichua siri ya mwanaye kwa kusema, aliwahi kuvaa jezi za Manchester United zilizoandikwa jina la Cristiano Ronaldo.

Fayza Lamari, mama wa nyota huyo wa PSG na Timu ya Taifa ya Ufaransa amekuwa akizungumzia mapenzi ya mwanaye kwenye mchezo wa soka tangu akiwa mdogo na kueleza aina mbalimbali za viatu alivyokuwa akivaa.

AC Milan, Real Madrid, Paris Saint-Germain, na Rennes zilikuwa klabu zingine ambazo Mbappe alikuwa na jezi zake akiwa mdogo.

Mbappe, ambaye alijiunga na klabu ya AS Bondy yenye maskani yake Paris akiwa na umri wa miaka sita, alipenda sana soka tangu akiwa mdogo sana huku Lamari akielezea jinsi uchaguzi wake wa jezi na ushabiki wa jumla ulivyochochewa na washambuliaji wakubwa wakati wa utoto wake katika miaka ya 2000.

Lamari amesema kuhusu jezi ya mwanaye ya AC Milan: “Aliivaa kwa mazoezi na hata kitandani. Lakini kama wengine wengi, Real Madrid, Ufaransa, PSG, Manchester United kwa CR7 alizipenda.

“Alipenda washambuliaji wa hali ya juu, lakini pia angeweza kuvaa jezi ya mshambuliaji wa Uswisi Alexander Frei wa Rennes.”

Lamari ameendelea: “Yeye ni mtoto wa wanamichezo, lakini alikuwa amezama katika kuishangilia AC Milan tangu mwanzo. Alipofika nyumbani, angezungumza tu kuhusu AC Milan.

“AC Milan ikishindwa, angeweza kutupa rimoti kwenye TV na kusema maneno machache mabaya kwa Kiitaliano.”

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii