Barca na City washinda mechi za awali za Champions

Manchester City ikiongozwa na Erling Haaland ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Young Boys na kuongoza kundi G, ikifuatiwa na RB Leipzig iliyopata ushindi dhidi ya Red Star Belgrade.

Mabingwa watetezi wa michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya, Manchester City wameanza vyema mbio za ubingwa sambamba na Barcelona na kuinyemelea hatua ya makundi.

Manchester City ikiongozwa na Erling Haaland ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Young Boys na kuongoza kundi G, ikifuatiwa na RB Leipzig iliyopata ushindi dhidi ya Red Star Belgrade.

Barcelona, iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Shakhtar Donesk katika kundi H, huku Porto ikiifunga Royal Antwerp mabao 4-1.

Ushindi huu unawaongezea matumaini kwenye mechi za mwisho wa wiki, wakati Barcelona itakapokwaana na Real Madrid katika La Liga Classico na Man City dhidi ya Manchester United katika Derby ya PL.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii