S2Kizzy athibitisha kufanya ngoma na Rihanna "Soon itatoka"

Mtayarishaji wa muziki Bongo, S2Kizzy amethibitisha kufanya kazi na Rihanna na kusema wimbo huo ukiwa tayari watu watausikia.


Miezi michache iliyopita, S2kizzy alisema kwamba yeye ndiye mtu wa kwanza kuwahi kutokea kutoka ukanda wa Afrika mashariki kushiriki katika mradi mmoja na staa kutoka Barbados, Rihanna.


Producer huyo baadaye alihariri ujumbe huo na kutoa jina la Rihanna ambapo aliweka emoji za mduara wa dunia badala yake, na hili limewatatanisha watu wengi kushindwa kuelewa alichokuwa akimaanishi awali kwa kuweka jina la Rihanna.


“Mtu wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kuwa katika kazi ya msanii Rihanna,” ujumbe wa kwanza kabla kuhariri ulisoma.


“Mtu wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kuwa katika project hiyo,” ujumbe wa pili baada ya kuhariri ulisoma.


Baada ya kuliondoa jina la Rihanna kwenye post yake hiyo, wengi wamesema labda ni kiki tu alikuwa anatafuta kwa kujizolea uhodari kwa kuwa wengi wanamjua Rihanna kama msanii wa kimataifa anayetamba mno.


Je, wewe unahisi S2kizzy alikuwa anamaanisha nini awali kusema ako katika ‘project’ ya Rihanna na kisha baadae kulitoa jina la staa huyo wa kimataifa?


Utakumbuka Rihanna anayefanya muziki wake Marekani, ni mshindi wa tuzo tisa za Grammy

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii