Kinda wa miaka 17 aiokoa FC Barcelona

Kinda wa FC Barcelona Marc Guiu ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga bao kwenye mchezo wake wa kwanza kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo kwenye Ligi kuu Hispania La Liga. Ameweka rekodi hiyo baada ya kufunga bao kwenye mchezo dhidi ya Athletic Bilbao.

Guiu alifunga bao pekee la mchezo huo dakika ya 80 ya mchezo na amefunga bao hilo kwenye mpira wake wa kwanza kugusa uwanjani, amefunga bao akiwa na umri wa miaka 17 na siku 291 na kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga bao kwenye La Liga kwa FC Barcelona kwenye karne 21.

Bao hilo la pekee lililoifanya Barcelona iibuke na ushindi wa bao 1-0 imeifanya timu hiyo kuweka rekodi ya kuwa imechecheza michezo 8 mfululizo bila ya kufungwa dhidi ya Bilbao. Kwenye michezo hiyo 8 wameshinda michezo 7 na wametoka sare mchezo 1.

Kufuatia ushindi huu Barcelona imefikisha alama 24 kwenye michtzo 10 wapo nafasi ya 3 ikiwa ni tofauti ya alama 1 dhidi ya Real Madrid wanaoongoza Ligi na Girona walionafasi ya pili wote wakiwa na alama 25.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii