Bosi Tottenham Hotspur afichua usajili wa Kane

Bosi wa Tottenham Hotspur, Daniel Levy amesema wameweka kipengele cha kumrudisha Mshambuliaji, Harry Kane kwenye kikosi chao, endapo FC Bayern Munich itachoka huduma yake na kutaka kumuuza.

Mwenyekiti huyo wa Spurs, Levy alifichua hilo kwenye jukwaa la mashabiki juzi Jumanne (Septemba 19).

Kane mwenye umri wa miaka 30, aliachana na klabu yake hiyo ya tangu enzi za utoto na kujiunga na FC Bayern Munich kwa ada ya Pauni 100 milioni.

Hilo lilihitimisha miaka mingi ya Kane kwenye kikosi cha Spurs, ambapo alifunga mabao 280 katika mechi 435. Na bosi Levy amedai kwamba Spurs bado inampa heshima kubwa Mshambuliaji huyo gwiji.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii