Mzozo kati ya timu ya soka ya wanawake ya Uhispania na Shirikisho la Soka la Kifalme la Uhispania (RFEF) unaonekana kufikia muafaka baada ya pande hizo mbili, pamoja na Baraza Kuu la Michezo la serikali (CSD), kufikia msururu wa makubaliano.
Mapema wiki hii, wachezaji 20 waliotajwa kwenye kikosi cha timu ya taifa walikariri kukataa kwao kucheza mechi mbili zijazo za UEFA Women Nations League, ikiwemo dhidi ya Uswidi siku ya Ijumaa.
Hata hivyo, wachezaji 21 kati ya 23 waliochaguliwa kwenye kikosi kwa ajili ya michezo ijayo sasa wamekubali kucheza na watasafiri hadi Sweden, kwa mujibu wa taarifa ya Rais wa CSD, VĂctor Francos.