Mashabiki Wanne wa Timu ya Namungo Wafariki Dunia Wakisafiri Kuishangilia Timu yao

Uongozi wa Namungo FC umesema gari walilokuwa wanatumia mashabiki wa timu hiyo kutoka Ruangwa kuja Dar es Salaam kuishangilia timu yao ikicheza dhidi ya Yanga mechi ya Ligi Kuu leo Septemba 20 saa 1:00 usiku limepata ajali eneo la Miteja karibu na Somanga mkoani Lindi.

Uongozi huo umesema mashabiki wanne wamefariki dunia na majeruhi ni 16 ambao wamepelekwa katika kituo cha afya Tingi wilayani Kilwa kupatiwa matibabu.

"Uongozi tunatoa pole kwa Wanaruangwa, mashabiki, familia na kwa wote waliopata ajali hiyo," imeeleza taarifa

Mechi ya Yanga na Namungo itapigwa katika uwanja wa Azam Complex.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii