Ten Hag alalamikia solo la usajili

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag, amelaumu timu zinazopandisha bei ya wachezaji kwenye soko la usajili wakati klabu hiyo ya Old Trafford inavutiwa.

Ikiwa ni pamoja na nyongeza mbalimbali, United ilitumia zaidi ya pauni milioni 180 kununua wachezaji wanne wapya, pamoja na kumsajili Jonny Evans kwa uhamisho wa bure.

Walipolaumiwa kwa matumizi makubwa katika majira ya joto, ikilinganishwa na timu ya Brighton iliyoondoka Old Trafford Jumamosi (Septemba 16) na ushindi mnono wa 3-1, Ten Hag alipuuza.

“Nadhani timu zote zinatumia fedha nyingi” alisema.

“Hiyo ni kweli kwa klabu nyingi kama Chelsea, Liverpool, Manchester City, Arsenal, Newcastle United na hata West Ham.

“Brighton pia walitumia zaidi ya pauni milioni 80, lakini kwa hakika walileta karibu faida ya Pauni Milioni 100 katika ada za uhamisho kutoka kwa wachezaji walionunuliwa hapo awali kwa bei nafuu ambao waliwauza kwa gharama kubwa.”

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii