Kiongozi wa upinzani azinduwa kampeni ya uchaguzi Liberia

Joseph Boakai, amezindua kampeni yake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba, ambapo atachuana na nyota wa zamani wa soka na rais wa nchi hiyo, George Weah.

Kiongozi wa upinzani nchini Liberia, Joseph Boakai, amezindua kampeni yake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba, ambapo atachuana na nyota wa zamani wa soka na rais wa nchi hiyo,George Weah, baada ya muhula wa kwanza uliogubikwa na majanga.

Maelfu ya watu ambao ni wafuasi wa Boakia mwenye umri wa miaka 78, ambaye aliibuka katika nafasi ya pili katika uchaguzi wa mwaka 2017, walikusanyika katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia, jana Jumapili na kumuunga mkono mgombea wao huku wakipeperusha bendera na wakipaza sauti kudai mabadiliko.

Katika mkusanyiko huo, walihudhuria pia baadhi ya mashabiki wa zamani wa Weah ambao wamekatishwa tamaa na kubaini kuwa ameshindwa kuboresha hali ya maisha, kukabiliana na mfumuko wa bei za bidhaa na kutokomeza ufisadi katika nchi hiyo masikini ya Afrika Magharibi ambayo katika karne hii, ilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, janga la maradhi ya Ebola.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii