Kufungwa miaka miwili kwa kujichua ndani ya Ndege

Rapa na muimbaji wa Marekani Desiigner yupo kwenye kifungo cha nje na uangalizi kwa miaka miwili, kufanya kazi za kijamii na kulipa faini ya Tsh Milioni 12,525,000 kwa kosa la kujichua 'Masturbation' ndani ya ndege.

Hitmaker huyo wa ngoma ya Panda ameamriwa na Mahakama ya Wilaya ya Minneapolis Marekani kama mkosaji wa ngono kwa kitendo hicho alichofanya mwezi April.

Pia katika kifungo hicho anatakiwa kupimwa afya yake ya akili, atachunguzwa kuhusu utumiaji wa madawa ya kulevya na kupigwa marufuku kumiliki silaha yoyote.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii