Uhispania, Morocco na Ureno kuwa wenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2030

Morocco, Uhispania na Ureno zimetajwa kuwa wenyeji wa Kombe la Dunia la soka mwaka  2030, huku Uruguay, Argentina na Paraguay wakiwa wenyeji wa mechi za ufunguzi kuadhimisha miaka 100 ya mashindano hayo, shirikisho la soka duniani FIFA lilisema katika tangazo la mshangao siku ya Jumatano.

FIFA ilisema zabuni ya pamoja kutoka kwa Morocco, Ureno na Uhispania ndio wagombea pekee wa kuandaa mashindano hayo. FIFA walipaswa kutangaza waandaaji mwaka ujao.

Kombe la kwanza la Dunia mwaka 1930 lilifanyika nchini Uruguay na na wenyeji kushinda baada ya kuwashinda Argentina katika fainali huko Montevideo.

Uhispania imetunukiwa Kombe la Dunia wiki kadhaa baada ya mkuu wao wa zamani Luis Rubiales kulazimishwa kuachia ngazi kufuatia kumbusu mdomoni mchezaji Jenni Hermoso katika Kombe la Dunia la Wanawake.

Uamuzi huu wa Jumatano wa FIFA ni mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kupangwa katika mabara matatu na nchi sita, ambayo inaweza kumaanisha mechi za makundi zitalazimika kufanywa katika misimu tofauti kulingana na eneo la Dunia waliopo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii