Mwanasheria afichua siri za Mohamed Salah

Mwanasheria na mshauri wa Mshambuliaji Mohamed Salah amedokeza  kuwa nyota huyo wa Liverpool anaweza kuwa anapata kiasi kikubwa mno cha mapato ya jumla kwa mujibu wa The Guardian.

Rammy Abbas Issa aliripotiwa kuwaambia watafiti wa Shule ya Biashara ya Harvard Business School ‘HBS’ kwamba kiasi hicho cha fedha kitakuwa matarajio ya kihafidhina kwa yota huyo wa Misri.

Issa pia alifunguka jinsi Salah alivyokaribia kuondoka kwa wababe hao wa Ligi Kuu kabla ya kuweka mustakabali wake klabuni hapo kwa kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu.

Salah alikuwa ameingia miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake na kulikuwa na wasiwasi kwamba angeondoka baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo kushindikana. Lakini, Mshambuliaji huyo wa Misri alisaini mkataba mpya Julai 2022 akijitolea kukaa Liverpool hadi Juni 2025.

Issa sasa amefichua kwamba mkataba mpya wa Salah pamoja na stahiki nyingine utamfanya apate pauni milioni moja kwa wiki. Kwa mujibu wa The Guardian, Issa alisema: “Unapokuwa umeweka maombi yako mezani na hupati chochote ulichoomba, unapaswa kuanza kufikiria kuhusu kuachana.”


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii